Sintah.Com Launched

Karibu Sintah.Com. Bonyeza Hapa Kuingia Sintah.Com

SEREKALI IKO WAPI??

wadau


nina rafiki yangu wa siku nyingi sana,kama mnakumbuka kuna siku jokate aliweka katika fb yake kuhusiana na mtoto aliyebakwa,huyu mtoto ni wa rafiki yetu Ms Dorah.


mdau
nilikasirishwa sana niliposikia hii kesi,ila nikajua serekali inachukua nafasi yake,
ni mtoto wa miaka minne amebakwa na dereva wa bajaji,hivi huyu dereva ana akili timamu au?
; kibaya zaidi kila siku wanapigwa kalenda katika kituo cha polisi kesi bado haijaenda mahakamani eti wanapeleleza, sasa wanapeleleza nini nawakati vipimo vipo sahihi kutoka kwa doctor kwamba amebakwa,na kikubwa zaidi huyo bajaji boy ndio alikuwa akimpeleka  shule kila siku, mama akajua ni mtu mzuri tuu,kumbe akageuza kibao, pale mum alipoenda Nai kikazi.

wamempima HIV hana wanatakiwa warudi tena after three months for checkup.


nini kifanyike wapenzi ili tumsaidie huyu mama na mtoto wake


serekali iko wapi?mpaka sasa kesi haijaenda mahakamani ni kwanini?rushwa au nini zaidi?


naandika this post na machungu zaidi coz i know how she feels right now.


God this is my country but i dont understand its system,this idiot should roat in prison.


naombeni mawazo yenu maana yatatusaidia sisi watu wake wa karibu.

16 comments:

Anonymous said...

pamoja na nia njema mnayozungumzia. Kuna sheria ya kulinda watoto wanaonajisiwa , kunyanyaswa. Ni kosa kutoa picha ya mtoto huyo bila kuidhibiti(distosheni) ili kuficha wajihi wake.Hili ni kosa kubwa ulilofanya unaua future ya huyu mtoto na kanuni za kitaifa na kimataifa zinahitaji ufiche sura yake.tafadhali mtendee vyema mtoto huyu tayari ameshapata madhara.

Anonymous said...

PS please toa picha ya mtoto aliyebakwa ni unafanya udhalilishaji it is a crime also.kisheria inampasa mtoto(victim) asiionyeshwe kwenye picha ndo maana hata wale watoto wa kesi ya babu seya hatujawaona hata kidogo.hata magazeti ya udaku wanayajua hayo.hata kama mama wa mtoto kakuambia uweke kwa kuwa na uelewa finyu lakini baba mtoto au ndugu zake au hata vyombo vya kutetea haki ya mtoto ikikuona unaweza kufungwa PS.

Anonymous said...

sasa inakuwaje bado huyo bajaj boy anaendelea kumpeleka shule kila siku, kama si kumkabidhi mke rasmi.

Anonymous said...

Labda mie nimeelewa vibaya, nafikiri hiyo picha ni ya mama mzazi wa mtoto aliyedhalilishwa kijinsia sio ya mtoto. By the wy, hata hiyo picha ya mzazi usingeiweka sinta nafikiri inaweza kuzidisha unyonge kwa mhusika. Ni ushauri tu.

Anonymous said...

Hivi hawa polisi wanaakili kweli?unapeleza nn wakati doctor ameshasema kuwa mtt kabakwa na vipimo vipo?hiyo kesi iko kituo gani?tutafika kweli kwa style hii jamani?namshauri dada yangu Dorah akamuone OCD then amueleze kilichotokea,naimani atamsikia kama haijui hiyo kesi,na akiona mambo ni yale yale basi apande kwa boss wake yaani RPC,nampa pole sana dada Dorah,
Zach.

Cham said...

Hhapa ndo naposhindwa kuelewa hizi sera za kuttetea akina mama na watoto zinamaana gani kama kwa mtoto mdogo kama huyo wanashindwa kuonesha msimamo wao..Kikubwa hapo itakuwa wasimamizi wa hiyo ksi(askari) watakuwa wanakula rushwa so wanachelewesha ili imalizwe kabla ya kwenda mahakamani.Pole sana dada Dorah ila ikiwezekana jariibu kutafuta wakili wako kama bado hope atakusaidia kumfikisha mmahali panapohusika huyo mshenzi..

Infortainment said...

mh huyo mama mzuri kama mtoto wake... Sijasikia kuhusu wanasheria hapo vipi nadhan hao wangemsaidia sana na pia ajue unaeza ukanyimwa haki yako kwa 7bu ya jinsia yake so afanye mpango huo wa wanasheria kwanza

Anonymous said...

Kutoa picha ya mtoto ni kumdharirisha huyo mtoto, Je huyo dereva wa bajaji yupo chini ya ulinzi wa polisi au bado yupo mtaani anazidi kubaka watoto wengine?????????????

Anonymous said...

pole sana,ila yote ni mitihani ya Mungu.kwa ushauli wangu aende pale LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTER pale Kinondoni Biafra anaweza pata msaada wa haraka.

jane bomba

Anonymous said...

Hivi wale watu wa ustawi wa jamii walioshughulika kwelikweli na ile kesi ya babu seya wako wapi? Nadhani kesi hii inafanana kabisa na ile kwa hiyo naona wafuatwe wakaambiwe hii ishu!

Anonymous said...

huyo mama akaonane nakina ananilea nkiya TGNP HAWA WATAMTETEA KWAHARAKA NA ATAIPATA HAKI YAKE MARA MOJA INAUMAA SAANAA....WAO KESI ZAKUPANDIKIZA WANAVYOZITOLEA MACHO KAMA ZAKINA SEA MBONA HIZI ZA UKWELI HAKUNA ANAYEJIGUSA????SHENZI KABISAAA

Anonymous said...

ktk cku zote leo ndyo umeweka mada ya maana pole kwa mama na mtoto

Anonymous said...

tafadhali washirikishwe wadau wa taasisi za kijinsia hasa TAMWA NA TGNP.watalifatilia kwa karibu hili jambo.inakera sana!

Anonymous said...

Aende Pia Ofisi za Tanzania Gender Networking Program (TGNP) pale Mabibo Sokoni atakutana na wakina Mama Ananilea Nkya,Dada Usu Mallya, Kijo Bisimba n.k atapata msaada wa kisheria pia anaweza kwenda ofisi za TANGANYIKA LAW SOCIETY KWA MSAADA WA SHERIA.

Anonymous said...

mh makuubwa

Anonymous said...

naomba kuhuliza uyo dereva uyko nje au?mna anatakiwa awekwe ndani kwa kweli uwo c uungwana hta kidgo na hapo ni rushwa ndo yatumika na sio kingne.