Sintah.Com Launched

Karibu Sintah.Com. Bonyeza Hapa Kuingia Sintah.Com

KAMA MAPENZI NDIO HAYA,NI BORA AWE SINGLE

kwako jlo bongo
natumaini hujambo na unaendelea kuchapa kazi,mimi nina swali na naomba wadau mnisaidie kulijibu hili swala
waungwana mapenzi ni magumu kila mtu anajua, eti inawezekana mtu unaempenda anakuja from no where anakwambia naomba tusionane kwa siku tatu?eti tukionanana
 kila siku tunazoeana vibaya sasa bora tupeane space ya siku 3 ili tukumbukane
je wadau mpenzi kama huyo utamuelewaje?

maoni yenu wadau yatasaidia kumsaidia huyu kaka
wasalaam

9 comments:

Anonymous said...

Hivi ndo vitu tunavitaka vya kushauriana. Hapa sasa umeanza kufanya mambo sio ule ushamba wa kujinadi na kutafuta umaarufu kwa nguvu zote.

Ushauri wangu kaka yangu huyo bi dada kwa kweli hakupendi maana mtu unayempenda unatamani uwe naye kila saa.

Anonymous said...

Angalia usijeukawa uko kwenye foleni anajaribu kupanga ratiba yake.

Anonymous said...

kaka labda anakazi nyingi jaribu kuangalia ugumu au wepesi wa kazi zake then utamhukumu

Anonymous said...

wewe mkaka utakuwa kinganganizi uwezi jua kwanini kakwambia hivyo tuliza mpira

Anonymous said...

For my side sijaona tatizo hapo labda anatingwa na kazi pi kama mdau hapo juu alivyosema, muhimu kumuelewa mwenzi wako..... ucfikirie anakusaliti koz aliwazalo mjinga............

Anonymous said...

Mwenzangu inawezekana hana hata kitu basi tu anataka space.

Mi nina boyfriend wangu kaniganda,sikatai ananipenda ila kutwa kucha yuko kwangu na anatakata tuonane kila siku.Ila kuna saa natamani privacy,natamani kukaa peke yangu na sina Agenda za siri so sometime mtu unahitaji space na pia ni vizuri mkikaa mbali kidogo unamiss mwenzio

Anonymous said...

Mdau aliyesema anajaribu kupanga ratiba yake, namuunga mkono asilimia 100. Mmmh......Mjini kuna mambo?

Elmmy

mama b' said...

Amini usiamini akufukuzae hakwambii toka, kaka kama vipi bora utafute m2 mwingine huyo lazima atakuwa na m2 anayekuwa naye katika cku tatu hizo ambazo hataki muonane.

Anonymous said...

kwa mtindo huo,,mmmmmmmm......mulika mwizi!!!!