Sintah.Com Launched

Karibu Sintah.Com. Bonyeza Hapa Kuingia Sintah.Com

NAOMBA MSAADA WA MAWAZO

From zenere 2011@yahoo.com
To prettysinta244@gmail.com


Hi Sintah

Mzima,mimi ni rafiki yako kwenye face book na mdau mkubwa wa PS blog,ila kwa leo nina tatizo kubwa tu,nipo kwenye dilemma nilikuwa na bf wangu tuliokaa nae more than six years,tunagombana,tunapatana,mwezi uliopita nikasikia kuwa anataka kuoa nikamuliza akakataa,akasema nisikilize watu nimsikilize yeye nikaamua kuacha.
Mara msichana mmoja nilikuwa nafanya kazi nae akazaa nae,mara mwezi huo huo dada mwingine akazaa pia motto wale wa pili nikimuuliza pia anakataa
Then the next week ikawa send off nayeye akaenda na mpaka saa saba za usiku tulikuwa tunawasiliana nae,on Friday nikapigiwa simu na rafiki yangu kuniambia kuwa jumamosi atafunga ndoa (bf)yaani nilidata sintah na nikimpigia simu hapokei wala msg hajibu
Jumapili baada ya ndoa akaweka picha ya pete zao na kuweka katika bbm na ikisindikizwa na status im married
Nikamwambia hongera akajibu thanks ila nimekumiss sana,nikashangaa sana Sintah nikaiuliza ana nini huyu mpaka Tuesday akaja ofisini na kuniambia ameoa kimakosa na mimi ndio chaguo lake na nafasi yangu ipo pale pale,sintah na wadau wa PS nisaidieni kwasababu nimechanganyikiwa

Kwa ushauri,maoni,kutuma habari,picha tuwasiliane prettysinta244@gmail.com

Naomba mumsaidie kwa ushauri afanyeje maana leo kwake,kesho kwako

22 comments:

Anonymous said...

Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.........pole sana shost! huyo mwanaume ni mmbwa. ni ngumu bt jst try to forget him atakupotezea mda tu, angejua we ndo chaguo lake angekuoa ww. usikubali kudanganyika na kuishi maisha ya kitumwa....he z already married n the whole world knows that...bt kama unataka kuwa kimada maisha yako yote nii juu yako. sisi tunakushauri tu bt uamuzi unao wewe

Anonymous said...

Ni kweli nafasi yako iko palepele, ya u-carpet. anazurura weeeeeeeeeeeeeeeee miguu anakuja kufutia kwako. wake up gal n thank GOD kwa kukuepusha na hilo gumegume...acha kuwa mpumbavu, evrythng z jst under ur nose bt yet unataka kuling'ang'ania jitu lisilo na utu...........

sintah said...

kwa mimi nakuomba dada ;;;;;;umuache huyo nguru papa,kumbuka kakudanganya kwanza kuhusu watoto,pili kuoa what else do you need?anakuonea haya kukwambia hakutaki just move on my love
siku hizi wanawake hatudanganyiki there plenty of opportunities are waiting
move on pal

Anonymous said...

mambo sinta? huna haja ya kupost hii....if its posibo toa email ya huyo dada hapo juu unless kama alikuruhusu uipost pia.........msaidie kwa hilo asije akawa talk of the town, najua amedata so its posibo alisahau kukwambia usipost email yake.DONT POST THIS MAANA ITALETA ATTENTION

Anonymous said...

MIMI NAKUSHAURI ACHANA NAYE HUYO NI KAMA MNYAMA HANA ROHO YA KIBINADAMU,ANATAKA AKUCHEZEE TU,AKIKUFATA TENA UMFUKUZE KABISA NA UMWAMBIE USIMUONE TENA,TULIA DADA YANGU MUNGU ATAKUPA MUME MWEMA HUYO HUKUPANGIWA NAYE,OMBA MUNGU UMSAHAU KABISA

Anonymous said...

Pole sasa nimeguswa mpaka ku-comment maana imeshanitokea na mimi jipe ujasiri achana na huyo mwanaume utaona mambo yote yakuwa sawa. Mwanzoni inakuwa ngumu unatamani hata uendelee kuwa nae akiwa tayari kwenye ndoa ila kadri siku zinavyoenda utazoea na kutotamani hata kukutana nae. ACHANA NA HUYO MWANAUME SI WAKO NA UNATAKIWA KUJUA YUPO ALIEANDALIWA KWA AJILI YAKO haujakutana nae!

sintah said...

jamani huyu dada ameomba nisitaje jina lake na email yake nimeiweka kuongezea vinamba tuu na nimechakachua si email kamil
so haina majotroo nyie msaidieni tuu wapendwa maana si wanaume magume gume

Anonymous said...

achana na huyo mwanaume hakupendi ww ndie unaempenda na ameshagundua hilo kwa hiyo dada jitahidi umtoe moyoni mwako achana nae kabisa na usiwe hata na mawasilian nae

Anonymous said...

Dada ndoa ni mpango wa Mungu na wala si wa kibinadamu, huyo mwanaume hakuwa mpango wa Mungu kwako hivyo mshirikishe Mungu nia yako juu ya kupata mume mwema na wakweli, na Mungu atakujibu. pole sana

Anonymous said...

mh pole mdada huyo hakufai achana nae tena ucfikirie mara mbili,jipe moyo utampata wa ukweli

Anonymous said...

Achana nae kabisa, huyo hakufai hata kidogo ndugu utapoteza muda wako bure kumfikiria kama unaona vipi chukua likizo kidogo nenda nje ya mji uka relax ili upotezee. Hana mapenzi yakweli angekuwa anakupenda kwanini asingekuoa wewe? ndugu pole sana hayo mambo huwakumba kina dada wengi tu!! sio chaguo lako huyo Mungu kakuandalia zaidi yake, pole kwa kuupoteza muda wako sasa SONGA MBELE SAHAU YA NYUMA.

Anonymous said...

Yaani we dada nimesikitika sana kwa hili lililokukuta kwakweli...mpaka nimepata hasira za kumpiga huyo mwanaume. You know what rafiki, "HE DOESNT DESERVE YOU" Mimi yalishawahi kunikuta kama yako, nikajiulizauliza mara mbili nikasema NILIKUJA DUNIANI PEKE YANGU KUPITIA WAZAZI WANGU, HUYU MTU NILIYEKUTANA NAE UKUBWANI ASI-DEFINE HOW MYLIFE WILL BE......NILIMUACHA NIKAENDELEA MBELE NA SASA NINA FURAHA....USIOGOPE HAITAKUWA MWISHO WA DUNIA ACHANA NAE KABISA...TENA SIKU NYINGINE AKIJA KUKUFUATA OFISINI MWAMBIE HUNA TABIA YA KULA CHOO KUBWA IKISHATOKA MWILINI.

HANA LOLOTE HUYO...HE IS JUST A LOSER...MPOTEZEE TENA HARAKA SANA

Anonymous said...

ACHANA NAE KABISA,nakushauri tulia kwanza then angalia mbele,si mkweli hata kidogo ni tapeli wa mapenzi then mshamba hata huyo aliemuoa hana mapenzinae ya dhati atakuja kumuacha solemba angalli ameingia ndani ya ndoa bora mola kakuepushia maana hilo ni balaa.fanya kaziyako angalia life yako ipo siku utampata anaekupenda kupita kiasi,pole ni cha changamoto katika maisha wengi uwa yanawakuta hasa wanawake kuwa makini

Anonymous said...

Mwaya huyo hana lolo zaidi yakukupumzikia!!!maradhi kila kona,mshukuru mungu kwan kakuepusha na msalaba mzito wa maisha yako!!i blive there is someone for you!!!its just the matter of time,kamata time yako lisongeshe life!!!huyo si mtu bali ni jitu!!mana kama angekua na utu asingefanya yote hayo!!angekua na utu,there is no love there rather tha desire!!!fumbua machona umwombe mungu kwan wawezakua unang'ang'ania donda la maisha!!!pole sana ma dear!!

Anonymous said...

Dada yangu mpe maisha yako mungu utapata mwingine anayekupenda kwa dhati huyo anataka kukuchezea tu

Anonymous said...

Pole sana rafiki but jipe moyo msahau kabisa huyo mwanaume si chaguo lako mkabidhi Mungu matatizo yako nae atakushindia kuwa busy na kazi yako dada usijerudia kosa huyo sio mtu kabisa tena pole yake aliyeolewa naye shukuru Mungu amekuepusha nae maana hata huyo aliyeolewa nae nahisi kalazimisha kuolewa POLE SANA ni mapito tu hayo utampata wa kwako mwenye mapenzi ya kweli

Anonymous said...

mmmh! pole sana mwayego mmmh! mana haya yantoke akila siku my dia take it easy lol.... me jana nimejiwekea single kabisa na nimeshaliacha mana lijitu limeowa sasa mnafanya nini zaidi ya kupotezeana muda tu

Anonymous said...

UNAHITAJI USHAURI GANI TENA, NA MWENYEWE UMESHAYAONA. HEBU JIPANGE WEWE KWANI MWANAUME MMOJA.

Anonymous said...

unless otherwise you are a cheating skunk......sioni kilichokuchanganya hapo.....ameshaoa halafu unauliza tena!!!??? you should know better......wanaojijua wana thamani hawahitaji hata ushauri wa mtu kwasabau ni jambo liko wazi kabisa kuwa huwezi kuwa na uhusiano na mume wa mtu......MOVE ON.....kwani yeye ndo mwanaume peke yake duniani!!!???? Afie mbali huyo tena asikushushie hadhi yako kabisa......umemjua kwa miaka sita tu halafu akiletee za kuleta!!!???? we dada tafadhali chondechonde usijaribu kumkubali tena.

Huwezi jua Mungu amekuepushia kitu gani. Kuna siku nilikuwa naangalia Oprah akasema ikitokea mwanamke umeachwa na bf au mchumba wala huna haja ya kulia otherwise you should say HALELUYA asante Mungu kwa kunilinda.Angekuwa ni wako ambaye Mungu amekupangia asingeenda kuoa mwingine. GOD WILL MAKE VEVRYTHING BEAUTIFUL IN HIS TIME. So worry not rafiki.

Anonymous said...

mumie achana nae huyo tapeli,,, ndivo walivyo hata wakioa wanajifanya ww ndio chaguo lako kama ni chaguo na nafac ipo pale pale c angekuoa ww!!!!! Ucfanye nae communication ya aina yoyote ile mpenzi.mpotezee mazima. Pole pia darling cpendagi mwanamke mwenzangu awe disturbed na mwanaume nakwazika.. pole sana...

khadija said...

yaani hapa nilipo natetemeka mikono yaani hayo yalishanitokea mimi tena shoga nilizchwa na mimba ya miezi miwili na nusu. mwanaume akaondoka mimba sikuitoa na mpaka sasa nina mtoto wangu wa kiume mzuriii tu lenyewe nilishalidelete moyoni na machoni. hujachelewa dada tupia kule hiyo takataka ya manispaaaa, msonyoooooooo wake nishampa huyo firinyiti mchambia vijiti...

Anonymous said...

Haingii akilini mwanaume aende akaoe mwanamke mwingine halafu aendelee kuja na ofisini kwako kukuambia muendelee. Lazima wewe ulikuwa ''spare tyre'' kwa miaka yote hiyo sita unayosema.

Yaani alikuwa anakufanya wewe poozeo, na ulikuwa unajua hilo ila ulikuwa tu unajitoa ufahamu! Hebu amka, rudi kwenye akili zako (go back to your senses) na ujiangalie upya!

Nina uhakika huyo mwanaume akija hapa akaelezea upande wake wa shilingi watu watapata picha halisi ya ni nini kilitokea! Haiwezekani mwanaume akawa na roho ngumu kiasi hicho!