Dada PS
Kuna mambo nataka ni waeleze watu kuhusu ma house girl
1. House girl
huyu ni msichana anaefanya kazi kwajibikaji,anawahi kuamka, anafanya usafi anaandaa maji ya kuoga,anapika chai,anachota maji hata umbali wa kio meter tano
2.Yaya
Kila kazi lazima aagizwe kama sivyo hafanyi,mara nyingi akikaa jikoni hatoki mpaka afokewe,huwa anakula jikoni,chakula chake kinakuwa ndani ya sufuria tuu na si msafi
3.Msichana wa kazi
Maisha yake kama mzaliwa wa familia anavaa kisistaduu,simu kila wakati,anafanya kazi zake haraka ili aoge,avae,ajipodoe na kukaa kibarazani kusubiri vijana wasio na kazi mtaani wapiti na kumtongoza
Je mpenzi wa PS unamtaka nani kati ya hao akae na nyumba yako?
Ni mimi
Mdau bongoland
No comments:
Post a Comment