Sintah.Com Launched

Karibu Sintah.Com. Bonyeza Hapa Kuingia Sintah.Com

TUWE MAKINI SANA NA UTANDAWAZI

Ndugu zangu napenda kuwashirikisha kisa hiki ili juu  ya wanaume wa kwenye Internate na wanawake wa kwenye Internate.
Rafiki yangu jina si harisi Vick alinisimulia kuwa alipata mchumba wa kizungu kupitia mtandao wa furani. Mmh! nilitapata mstuka sana nikajalibu kumdadisi ni kweli hizi habari? Akanihakikishia ni kweli na sasa huyo mzungu anajipanga kuja, huyo rafiki (mchumba) anaishi UK. Akaniambia pia wanawasiliana  wanaongea naye na simu kila siku au kutumiana sms, na akaniambia amemwelekeza hadi jimbo analokaa na mtaa na no. ya nyumba. Pia amemtumia kopy ya pasport. Nikamuuliza picha ya kwenye passport ni sawa na hiyo aliyoiweka kwenye huwo mtandao akaniambia ni sawa hata picha zingine kamtumia sura ni moja,. Nikawa very interest kujua nini kitaendele, Siku zikapita Vick akaniambi mchumba wake anataka copy ya passport yake imsaidie kupata Visa ya kuja .
Huyo jamaa akampigia Vick kuwa ameshapata Visa atakuja Tz baada ya siku kadhaa maana anaenda kwanza Bangladesh kapata tenda ya ujenzi anaenda kunegotiate  na Client  wake  juu ya malipo, Yeye ni mkandalasi wa majengo anavyodai. Vick alifurahi sana akanipigia kunieleza jumapili mchana mheshimiwa anaingia naomba unisindikize kumpokea. Nikamwambia sawa lakini moyo wangu bado hauamini. Jumapili ilifika muheshimiwa hatujamwona. Muda si mrefu akampigia simu Vick code na No.ni nyingine tukaamini kweli yupo Bangladesh. Akamwambia Vick tafadhari nimekwama hapa nipo hotel nimeshindwa kusafiri maana Air port wanataka nionyeshe show money.  Kadi  yangu nimeisahau Uk. Sina hata shilingi kumi hapa na nahitaji kufika Tz, Tafadhali nitumie USD.2000 nifike tuonane. Nikirudi tu Home Uk nitakurudishia. Mmh! Moyo wangu ukasita tena Vick akawa na mchecheto wa kuzituma hizo pesa, nikamwambia usitume pesa maana huyu mtu amekwambia yeye ni mkandalasi inamaana huyo Tajiri wake ameshindwa kumpa hata Advance au kumweleza kilichomsibu akamsaidia? Vick hakutaka tena kushare na mimi mambo yake tena, kesho yake akatoa pesa yake Benk na akakopa pesa zingine ili amtumie muheshimiwa bila kunishilikisha.
Siku zikapita muheshimiwa hatokei, Vick uzalendo ukamshinda akaja kunieleza nimetapeliwa Yule jamaa nilimtumia pesa hajaja kila nikiingia online namwona na nikimuuliza vipi mbona huji ananiambia amezuiliwa hotelin maana anadaiwa pesa na kwa sasa yeye hana tena pesa. Mpaka arudi Uk. Ninayoongea ni miezi 7 sasa imepita huyu mtu amadai bado hajafanikiwa kuondoka. Nikamwambia Vick Kuwa makini katika maamuzi usipende
  kumuwamini mtu hata wazungu wengi ni matepeli.

asante mdau uliyetuma hii kwa niaba ya prettysintah blog
IT Dept

14 comments:

Anonymous said...

she is a fool to do that na believe huyo sio mzungu ila katumia identity ya mzungu.hatakua mnigeria kabisa.my friend was in a same situation.OMG

Anonymous said...

wanaijeria hao hamna cha mzungu wala mhindi. kuweni makini huku nje wapo wengi sana tu. namba za simu wanajua wenyewe wanavyozibadilisha UK code na code ya nchi yeyote unapata. kazi kwenu wenye tamaa

Anonymous said...

wale wanaoshobokea kuolewa nje bila mpangilio na bado

Anonymous said...

pole dear,,,nipo sweden yalinikuta....nikawa nachemka sana kutaka kutuma....uzuri wa kumshirikisha best yako ndio huu....best yangu akasema ..poa usiende pupa....itakuwa utapeli...kweli nilimsikiliza..baada ya kuendelea ku-kontakt naye....nikagunduka speech yake nikama ya ki-naigeria...

machale yakashtuka mapemaa....hakupata hata senti.....he have done a good business...kwani atakuwa amewashika wengi tuuu.....pole dada!!

Anonymous said...

nyoooooooooooo!hizo pesa angekuomba mamako ungempa? ndio ukome.tamaa mbaya

Anonymous said...

haahahahahaha! jamani tena muwe makini kabisa mana mwingine anaji9fanya amekutumia parcel kwa courie inayojulikana kama cepacity! at the end...kutuma atume yeye ati kulipia ulipie wewe mtumiwa...yani nahisi wamshawaliza wengi!!!! tetetetete! be ware gels!

Anonymous said...

mmmmh wapopo hao( Nigerian's) washamuuingiza mjini pole shoga

Anonymous said...

sintah ata ukibana usibane shauri yako ila hii issue ni wewe wala sio nani wala nani na nina uhakika asilimia mia tatu looh yamekukuta unajifanya unatoa ushauri wakati ni wewe mwenyewe wadau asiwazingue yeye ndio aliyeingizwa KING na tamaa zake

IT said...

wewe una akili fupi alikwambia nani sintah anaingizwa mjini kiajabu hivyo?au umesahau kwamba yeye ni mpare halisi na hana muda na wanaume wa internet au wanaume wengine maana ana bf wake anampenda sana na hana tamaa za kijinga muacheni sintah anajilia bata sasa wewe endelea kupaka matope wakati yeye sasa yupo diplomatic delegation

Anonymous said...

huyo tapel mkubwa hata mimi alitka kunitokea ila nimlishtukia na aliomba nitume kiasi ya pesa lakni sikufanya hivyo..na mmoja anaitwa Mbongeni George Sibeko namba yake ya simu inaishia na 163, nao waliomba niwatumie pesa kwani jamaa amekamatwa kwa kubeba kiasi kingi cha pesa,anadai yy naye anafanya kwa agro product and real estate..naye alikuwa anapita Asia kwanza ila alipata matatizo SA..lol i didnt send the money..pole mpendwa sometym tafakari ushauri unaopewa na rafikizo

Anonymous said...

Na sio wanigeria tu pia waghana ndio zao matapeli sana hawa jamaa, pole sana Shoga ila ushapa fundisho siku nyengine hutapeliki.

Anonymous said...

Hah! Kuna kina dada wa Tanzania wanatamani sana kupata wapenzi/waume wazungu basi mbinu wanazotumia utawaonea huruma! Ona kama huyu alivyoingizwa mjini!

Na wewe unaye post kwa niaba ya Sintah basi uandike vizuri na kuedit kabla hujapost! Maneno yako yana makosa meengi saaana! Siyo "nikawa Interest", ila "nikawa Interested", pia ni "Halisi", na siyo "Harisi", ni "Kujaribu", an siyo "Kujalibu", ni "Mkandarasi", na siyo "Mkandalasi"!

Habari ikiwa na makosa mengi haipendezi, inakuwa kama imeandikwa na Lay man so inashusha Hadhi ya blog. Try hard to post error free informaton, hata kama ni bahati mbaya basi makosa yawe machache! Otherwise, you have posted an "lesson" information.

Anonymous said...

kweli ni synta

Anonymous said...

we dada mi naisi ni wewe