Sintah.Com Launched

Karibu Sintah.Com. Bonyeza Hapa Kuingia Sintah.Com

KUOLEWA NA MUME TAJIRI

Dada Ps

mim ni msichana wa miaka 20 natamani sana kuolewa na mwanaume tajiri ila watu wanasema wengi kuwa wanaume wengi matajiri wana wanawake wengi sana,hivi  mimi nitafanyaje?dada sintah naomba unishauri na wadau wa PS wote mnisaidie maana ho ndio ndoto yangu kubwa

ni mimi
Linda
Morroco

5 comments:

Anonymous said...

Umemaliza chuo? U cant be serious embu kaoge ukafanye assignment,Wenzako wanawaza kumaliza chuo wapate kazi nzuri we unawaza kuolewa na mtu tajiri??? shame on you tena nina mashaka na wewe unaweza kuwa ni beki tatu umepita humu kwa makosa..

xxxxx
Mdau Paris

Anonymous said...

annoymous hapo mbele umeongea la maana sana,wewe dada kwa haya maisha ya sasa unafikiri kweli swala la kuolewa na mtu tajiri?mimi binafsi nahisi una utindio wa ubongo

Am
Dar

PS said...

Hallow Mpenzi waPS blog
kuwa na akili ya kufumbua maneno na mambo hapa ktk blog utaona watu wanakukasirikia maana wengi wao utakuta wameathirika na hili swala tulia mdogo wangu au dada yangu
elimu ni ufunguo wa maisha waza kusoma zaidi
ni mimi
PS

Anonymous said...

Kwani wewe unchokitaka kwa huyo the so called "mwanaume tajiri" ni nini? Soma uweze kujinunulia kila kitu unachotaka sio kutegemea change kutoka kwa mwanaume. Wanaoolewa na matajiri kwa ajili ya pesa hawana raha. Baada ya kuzikinahi hela hizo then what? Libaba hili halijui kazi chumbani?

Mapenzi ya kwendi ndio foundation mdogo wangu na usijidanganye kuona hao wanawake walioolewa na matajiri wakienda sallon na kuendesha mgari ya kifahari nyumbani hawana saying kabisa na wanakalia kukatch upp na urembo wakiogopa yule mwanaume asiyeakaona mwanamke mwingine.

Mimi sasa hivi ni mtu mzima in my mid 30's na sijaolewa mpaka sasa hivi kwa vile ni kuwa nina dada wawili na mama wote waliolewa mapema sana na nikiwaangalia walikua na so much potentials kama sio kuolewa mapema. Kwa vile kwetu upande wa mama wana akili sana wajomba zangu na aunt yangu wote ni Phd holders na unajua tena ukiolewa bongo ni kuzaa na kuanza kutunza watoto...mama alikua wa kwanza akalazimishwa kuolewa na kuacha shule na kututunza sisi (thanks to her) But I feel for her.. my aunt yeye aliponea alikua miaka imeshabadilika na kwenda shule vizuri. Huwezi amini dada yangu mmoja saa hivi ndio amepata masters yake at 43 na aliolewa akiwa na O level education na mumewe alikua anamaliza Phd yake. Lakini baada ya kuona hapelekwi kwenye "party" za kioffice, safari za kikazi akaona huyu mtu labda ananiona sijasoma. Dada yangu ameanza kusoma polepole na sasa ana masters lakini najiuliza kama angesoma kwanza ndio akaolewa unapata mwanaume anayekuheshimu. ndio wana ndoa nzuri lakini saa nyingine nilikua naona kuna dharau fulani kutoka kwa shemeji..Nakumbuka nikiwa mdogo kitu kidogo utasikia shemeji akisema huyu dada yako hajui. Alikua tu hataki kusema elimu yake ni ndogo. Mambo kama hay nikikumbuka ndio yalikua yananifanya nijipange vizuri kabla sijaamua kusettle na sikutaka kuchukua that route at all...I wanted to first establish my name na sasa I am happily soon to be married but with my dignity na sio kama property tu.

Anonymous said...

we naona unadataaaaa hebu tafuta maisha yako kwanza...