Vodacom Kutoa Tuzo Kwa waandishi mahiri kumi wa mitandao ya jamii na tovuti Nchini.
· Waandishi wa mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na mafanikio yao.
· Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom”
Dar es Salaam,Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora
kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao.
Tuzo
hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”,
zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao
ikiwa ni kwa mala ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya
Vodacom.
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa
Waandishi wa mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa
taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
Wapo
waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala
mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja,
Ni kwa sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana
na mabadiliko waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
Baadhi
ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo
mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii, Kuzingatia ueledi
wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika
utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo
vingingine.
Waandishi
wa mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili
kuwawezesha kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
Kampuni
ya Vodacom Tanzania pia itaanzisha mfuko wa fedha wa maendeleo ya
digitali, Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza
umahiri na kuboresha kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.“Huu ni
mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika
udhamini na kuendeleza shughuli zao”, Alisema Meza na kuongeza kuwa, “
Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji waandishi wa mitandao ya
kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi tutaendelea kuthamini na
kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
Mwisho...
3 comments:
mchango wako unaeleweka Pretty wetu ni mmoja wa matop ten
jirani yako sijui kenda kwa mumewe kimya nyumbani hakuna mtu
eeeeeh yetu macho
Post a Comment